MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amewashangaza watu baada ya kutundika mtandaoni picha zinazomuonesha akioga bafuni huku nyingine akiwa maliwatoni.
Picha hizo zinapatikana kwenye mtandao wake na hakueleza ilikuwa wapi ila akasema
ilikuwa ni siku alipoamua kuitumia wikiendi yake ipasavyo katika hoteli ambayo hakuitaja jina.
![](http://4.bp.blogspot.com/-L2oFebpPFgg/U0DQwQE9nsI/AAAAAAAAROI/T_Z8QaSykvw/s640/didaakioga.jpg)
Baadhi
ya watu waliyoziona picha hizo walimponda wakidai eti ni ulimbukeni
lakini wapo waliomtetea kwa kusema, ni staili tu ya maisha aliyoamua
kuishi.
“Ushamba tu, ndo nini sasa? Angetuwekea ‘akikata gogo’ pia,” alisema mmoja wa wadau huku mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Dick akisema: “Msimuonee wivu mwenzenu,
anakula bata zake na nyie hamjakatazwa.”
Dida
alipoulizwa kuhusu kujianika hivyo alisema, hizo ni ishu zake binafsi
na wapenzi wake wanapenda kuona kila anachokifanya, ndiyo maana
anawawekea kwenye blogu yake
No comments:
Post a Comment